DJM

BENEDICT BANABA MNALIDJM/2024/0235

                     NYUMBA JUU YA JABALI

MAAJABU YA NYUMBA HIZI JUU YA MAWE

Mwanza ni moja kati ya majiji matano Tanzania,ambapo  limekuwa ni jiji la kustaajabisha na kuvutia kwa watu wengi kutokana na muonekano wake wa kuzungukwa na mengi na makubwa kiasi kwamba si ajabu kuona nyumba imejengwa juu ya mawe hayo

 NYUMBA IKIWA IMEJENGWA JUU YA MAWE
Lakini licha na kustaajabishwa kwa wageni wa jiji hili wao wenyewe wenyeji wa Mwanza kwao ni jambo la kawaida sana wala hawana hofu kama kukiwa na uwezekano wa mawe hayo kuporomoka kama wanavyozania watu wengine

NYUMBA IKIWA IMEJENGWA JUU NA KATIKATI YA MAWE

Maswali ya watu wengi hujiuliza kwamba ni gharama kiasi gani kupandisha mawe hayo juu ya mlima  ikiwa kuna umbali mrefu pamoja na namna ugumu wake ulivyo kwenye suala zima la uchimbaji wa shimo la choo.

MAWE YAKIWA YAMEBEBANA SAMBAMBA NA NYUMBA JUU YAKE
Uwezo wa mtu kujenga nyumba yake katika hii milima ya mawe basi ni wazi kuwa mtu huyo atakuwa na uwezo pamoja na nguvu ya kuupanda na kushuka kwani si jambo rahisi la kupanda hivyo vilima vyenye majabali makubwa tena yenye mapango ya kuhifadhia Wanyama wa kutisha kama vile nyoka na Wanyama wengine.

 HAKIKA NI MAAJABU YA KUVUTIA KATIKA JIJI HILI

Kweli ukistaajabu ya Musa basi utaona ya filauni na pia ule msemo usemao tembea uyaone hakika utaweza kujionea mengi kama ilivyo kwa wakati huu kwa nyumba nyingi ukizunguka hapa Mwanza zipo juu ya milima ya mawe. 

BENEDICT BANABA MNALIDJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALIDJM/2024/0235 Reviewed by Beatha on December 16, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.