MAKAZI MILIMANI NI KIVUTIO JIJINI MWANZA
Jiji la Mwanza ndio jiji la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ukiachana na Dar es Salaam, na sifa yake kubwa ni milima pamoja na miamba mikubwa ya mawe Rock City na kwenye hiyo milima kuna makazi ya watu wanaishi wamejenga nyumba tofauti na mikoa mingine ambayo utakuta watu hawajajenga milimani.kutokana na wakazi wa mwanza kujenga juu ya milima ya mawe imekuwa ni kivutio katika mkuoa wa mwanza na pia katika mikoa mingine.
Sehemu ya makazi ya watu katika Jiji la mwanza
Pia mwanza inaongoza kuwa na kabila la wasukuma na shughuli kubwa kwa mkoa wa mwanza ni kilimo Cha mpunga na uvuvi kwa kuwepo na ziwa kubwa linaloungunisha nchi tatu za Africa mashariki ziwa hilo ni ziwa Victoria .
Picha inayoosha Sehemu ya ziwa Victoria
Kingine kizuri hadi huduma za jamii zipo maji, umeme kuna sehemu hadi Daladala zinafika, kama umezoea kuona majengo marefu pekee yake ya Mwanza leo nakusogezea muonekano wa nyumba zilizojengwa juu ya mawe Mwanza.
Vilevile Jiji la mwanza asilimia kubwa wakazi wake nyumba zao wamezijenga juu ya miamba ambapo ni tofauti na mikoamingine na kufanya shughuli zao za Kila siku hivyo kuendesha maisha Yao kama kawaida kwa sababu maeneo ya milimani yanauzwa bei nafuu tofauti na maeneo ya kawaida
Kujenga nyumba juu ya miamba kuna hatari kubwa sana moja wapo ni kuanguka kwa nyumba na pia inaweza kusababisha vifo au ukilema kutokana na makazi kuwa juu ya miamba au kuhatarisha maisha kwa uwezekano wa kuwa na viumbe hatari kama vile nyoka mijusi inayokaa juu ya miamba .
Hakika mwanza ni Jiji zuri sana ambalo limebarikiwa miamba mingi na pia limebarikiwa kuwa na mandhari nzuri ambayo inapendeza machoni pa watu wengi.
Karibu Kanda ya ziwa karibu mwanza kwa kufanya utarii wa ndani na kuweka makazi pia

No comments: