Mpishi Bora wa kiume mtaa wa nyamalango mwenye miaka 29
Bwana Joseph chilambo mwenye umri wa miaka 29 anaye miliki mgahawa Bora wenye chakula kitamu chenye Radha nzuri na wateja kuvutiwa sana na chakula chake akitoa historia iliye mpelekea mpaka kuwa mpishi Mimi kabla ya kuwa mpishi nlikuwa nasoma chuo Cha sauti BAED nmesoma pale mpk nikamalza chuo na kugraduate lakini nilivo malizia tu Baba angu aliyekuwa akinisomesha alipoteza maisha Kwa ugojwa wa cancer nikakosa muelekeo ndipo nlpoamua kurudi nlipo soma niweze kuanza Biashara ambayo itanisaidia Mimi na wadogo zangu nyumbani
Akiwa ana hudumia wateja wake Kwa usafi
Pamoja na hayo kwanza nafurahia sana kazi yangu kwasababu ni kitu ambacho nilikuwa napenda japo cjakisomea japo wengi walinicheka na kunishangaa mwanaume na wezaje kupika lakini mi sijali kwasababu ni kazi inayo niingizia kipato
Akiwa anaandaa chakula Cha mchana Kwa ajili ya wateja wake
lakini ikitokea nikaitwa kuajiliwa ntaenda na ntawachia wadogo zangu wasimamie changamoto nazo pitia ni pale ambapo wanafunzi wa chuo wakifunga chuo miez kadhaa nakosa wateja na inanibidi nifunge mgahawa wangu
Pamoja na hayo nawashauli vijana wenzangu wasiogope swala la kupika ni la kawaida sana na linatusaidia kwenye maisha yetu ya Kila siku kupata kidogo Cha kuendesha familia
Reviewed by Deus
on
November 21, 2024
Rating:




No comments: