ULEMAVU SI UGONJWA
Kuna wimbi kubwa la watu nchini wenye Imani potofu juu ya watu wenye ulemavu,wakiamini kuwa watu wenye ulemavu hawastahili kupewa haki sawa na watu wasio na ulemavu,ambapo Imani hiyo imekuwa si ya kweli,kwani watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine wa kawaida,pengine watu wenye ulemavu wanastahili kupewa kipaumbele zaidi katika nyenzo mbalimbali.
Na leo hii kutana na kijana Francisco kimila mkazi wa nyamalango mwenye umri wa miaka 25 ni mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu Agustine mwenye changamoto ya ulemavu wa mkono pamoja na mguu,ambapo anatueleza mambo mbalimbali katika safari yake ya maisha hadi sasa,licha ya changamoto zote anazozipitia lakini bado hajakata tamaa katika kupambania ndoto zake.
Francisco kimila joachim
CHANGAMOTO ANAZOZIPITIA KIJANA FRANCISE
Katika upande wa changamoto anazozipitia Francisco ni pamoja na suala la ufuaji wa nguo zake,kwani kutokana na kutokamilika kwa mkono wake mmoja huwa anapata sana shida kuweza kufanikisha hilo,lakini kwa upande mwingine Francisco anasema kuwa haimletei shida sana kwani kutokana na uchangamfu wake na kushirikiana vizuri na watu basi baadhi yao huchukua jukumu hilo la kumfulia nguo zake.pamoja na ulemavu lakini pia amewashangaza wengi kwa uwezo wake wa kuendesha baiskeli bila ya mashaka yoyote yale.
UFANISI KATIKA KAZI ZAKE
Licha ya ulemavu aliokua nao kijana huyu,lakini pia anaweza kufanya kazi mbalimbali kama watu wengine,kama vile anaweza kuandika vizuri,kutembea kwa mguu mmoja bila kutumia magongo mbali na kuwa na changamoto ya ulemavu aliokuwa nao,na pia anaamini katika mipango ya mungu na kukubaliana na hali aliyokuwa nayo.
MAONI YA FRANCISE KWA JAMII
Kwanza kabisa jamii inabidi itambue umuhimu na thamani ya watu walemevu katika Maisha yetu na pia kuachana na Imani potofu za kutothamini mchango wetu.kwani walemavu ni watu wakawaida tu kama watu wengine.kwaiyo naomba kwa watu wote waendelee kutoa sapoti na ushirikiano kwetu kwani sapoti yenu ndio furaha yetu kwetu.
Reviewed by Yaywuwuwwu
on
November 21, 2024
Rating:




No comments: