CHOO BORA
Kwakuanza na maana ya neno "choo" maana yake ni chumba au mahali penye kifaa cha kuenda haja
Nyumba ni Choo ni kampeni ya usafi nchini Tanzania inayosimamiwa na wizara ya afya na ustawi wa Jamii yenye malengo ya kuhamasisha jamii katika kudumisha suala la usafi na ujenzi wa vyoo bora.
Choo Cha kudumu
kampeni hiyo inafanyika katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania. Ilizinduliwa tarehe 5 Juni 2012 na rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na baadaye katika awamu ya tano kampeni hiyo ilizinduliwa na aliyekuwa makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan mwaka 2016.
Malengo ya kampeni hii ilikua ni kuweka mpango mji ulioandaliwa na aliyekuwa rais wa awamu ya nne kuhakikisha Kila kaya au familia nchini Tanzania inakuwa na choo Cha kudumu kitakachoondoa mlipuko wa magonjwa holela yanayosababishwa na vyoo visivyokuwa vya kudumu.
Choo kisicho Cha kudumuMfano wa magojwa hayo ya holela yanayosababishwa na vyoo visivyokuwa vya kudumu kwa mfano kisonono, kipindupindu, kuhara na mengine mengi. Kwahiyo kampeni hii ililenga kukomesha au kupunguza milipuko hii ya magonjwa inavyoweza kusababishwa vyoo visivyo vya kudumu.
Kufuatia sababu hizo za kuanzishwa kwa kampeni hiyo pia wanchini wanashauliwa kuwa na matumizi sahihi ya vyoo pamoja na namna ya kuvitumia kwa kumwaga maji mengi ili kuondoa bakiteria wanaoweza kusalia na kusababishwa halufu mbaya pamoja na mlipuko wa magonjwa holela.
.
Reviewed by Christopha
on
November 21, 2024
Rating:



No comments: