DJM

DEUS B. THOMAS Djm/2024/1758

 

Kijana Anayejishughulisha Na Shughuli Ya Pikipiki (Bodaboda)


Pichani ni kijana mwenye umri wa miaka 28 Selemani Kahe Anayejishughulisha na shughuli ya kuendesha pikipiki katika kata ya Luchelele wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.

Selemani Kahe ni kijana mwenye umri wa miaka 28 anayejishughulisha na biashara ya kuendesha pikipiki (bodaboda) katika mtaa wa silivini wilayani nyamagana mkoani Mwanza. Anasema kazi ya boda alianza kuifanya miaka mitatu iliyopita na kapata mafanikio kupitia kazi yake.

ameeleza umhimu huyo pindi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa radio saut katika kipindi cha harakati za vijana, Seleman amesema kuwa moja ya mafanikio aliyoyapata ni Pamoja na kununua kiwanja ambacho analengo la kujenga nyumba yake Pamoja na familia yake japo kuwa kwa sasa bado anakaa kwenye nyumba za kupanga.



Aidha Selemani amesema nje na kazi ya bodaboda ni mhitimu wa chuo aliyesomea kozi ya ualimu na kutokana na kusubiri ajira ya akaamua aanze kujishughulisha na bodaboda.

    Mafanikio mengine ameeleza kuwa ameweza kuongeza wigo wa kufahamiana na watu hasa wateja wake na kupata uhakika wa kuingiza kipato kizuri kwa siku nzima

Lakini kazi hiyo ya pikipiki imekuwa na changamoto nyingi kwa upande wake, anasema kuwa kuna wakati biashara inakuwa ngumu pindi chuo kinapofungwa kwani wateja wake wengi ni wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino cha Tanzania kampasi ya Mwanza.

Licha ya kazi hiyo kuwa na changamoto nyingi, Selemani anawashauri vijana kujiingiza katika shughuli hiyo kwani ni shughuli halali na ni moja kati ya kazi ambayo ina manufaa.




DEUS B. THOMAS Djm/2024/1758 DEUS B. THOMAS Djm/2024/1758 Reviewed by Deus on November 21, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.