DJM

George Marwa DJM/2024/1972

Wanafunzi SAUT wakumbushwa usafi, ustaarabu
Moja ya maliwato ya SAUT ikiwa na kinyesi baada ya mwanafunzi kujisaidia na kuondoka bila kukisafisha. (Picha na George Marwa).


George Marwa DJM/2024/1972
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT) dewa ya Mwanza, wametakiwa kuzingatia usafi wa vyoo ili kuepuka mgonjwa ya kuambukiza ikiwemo kuhara na kipindupindu.

Rai hiyo ilitolewa jana na mmoja wa wafanya usafi chuoni hapo, wakati wakizungumzia tabia ya baadhi ya wanafunzi wanaojisaidia maliwatoni na kuondoka wameacha uchafu/ kinyesi bila kuundoa na maji ('kuflashi').

Mmoja wa wafanya usafi, Godliva Musiba alisema tabia hiyo isiyo ya kistaarabu inasababishwa na baadhi ya wanafunzi kutozingatia usafi licha ya kwamba wao kama wafanya kazi wanajitahidi kuimarisha usafi vyooni na katika mazingira ya chuo kwa ujumla.

"Baadhi ya wanafunzi wanatoka nyumbani na tabia zisizo nzuri, wanajisaidia na kuondoka wameacha kinyesi juu ya choo, unajiuliza huyu maana yake pia hakujitawaza wala kunawa mikono jambo ni hatari kwa afya yake mwenyewe na wanafunzi wenzake pia" alisema Musiba.

Baadhi ya wanafunzi wa SAUT akiwemo Esther John pamoja na Antony Juma walisema tabia hiyo inasababishwa na kukosekana kwa maji vyooni nyakati zote hivyo mwanafunzi kama amehemewa tumboni anaamua kujisaidia na kuondoka.

"Hata hivyo si ustaarabu kabisa, kama umekuta chooni hakuna maji, unaweza kuchukua ndoo na kufuata maji kwenye tenki nje, lakini vizuri kukuta choo kikiwa safi, unakichafua na kuondoka" alisema Juma.

Hivi karibuni baada ya chuo kufunguliwa, mmoja wa wanafunzi alibainika kuugua ugonjwa wa kipindupindu ambapo iliezwa kuwa alipata maambukizi hayo akiwa nyumbani hivyo ikiwa suala la usafi halitazingatiwa linaweza kuleta athari zaidi za kiafya kwa wanafunzi.

Itakumbukwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha suala la usafi hasa hata matumizi sahihi ya vyoo kupitia kampeni mbalimbali ikiwemo 'nyumba ni choo' pamoja na 'mtu ni afya', hivyo wanafunzi wa SAUT wakiwa ni miongoni mwa wananchi wanaosaka elimu wanapaswa kuwa mfano bora katika jamii kwa kuzingatia usafi.
Mmoja wa wafanya usafi SAUT akiweka maji kwenye ndoo kutoka kwenye tenki lililo jirani na vyoo kwa ajili ya kwenda kudanya usafi. (Picha na George Marwa).
George Marwa DJM/2024/1972 George Marwa DJM/2024/1972 Reviewed by BMG Media on November 21, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.