KAZI NI KAZI,KIKUBWA IWE HALALI
Idadi kubwa ya watu imekua ikiamini kwamba zipo kazi ambazo ni rasmi kwaajili ya wanaume na zipo ambazo ni rasmi kwaajili ya wanawake. Jamii imesahau kuwa kazi ni kazi haijalishi ni yakike au ya kiume ilimradi iwe halali na ikupatie kipato cha kukidhi mahitaji yako ya kila siku.
Watu wengi wanaamini kuwa kazi ya kusuka yaani kufanya kazi katika saloon ya kike ni kazi ya wanawake tu, leo hii nataka nikuondolee dhana hiyo baada ya kukutana na mwanaume aliyepata umaarufu katika eneo la Nganza kutokana na kazi yake ya kusuka.
Je!! Jamii inamchukuliaje?
Mtaalamu wa kusuka mitindo mbalimbali ya nywele, Hussen Idd akimsuka mteja katika saloon yake iliyopo eneo la Nganza jijini Mwanza.
Huseni Idd ni kijana ambaye anafanya kazi ya kusuka katika saloon ya kike takribani miaka mitano sasa, anaeleza changamoto zake na kusema, mara ya kwanza alipoanza kazi hii jamii haikumwelewa kabisa ilimshutumu kwa mambo mbalimbali mfano walimwona ni sawa na mwanamke, aliambiwa anajidharirisha yeye mwenyewe, familia na hata wanaume wenzake, alishutumiwa kuwa anatafuta nafasi nzuri ya kuwatongoza akina dada, pia ilileta vurugu kwa familia kwani familia ilidai kama hana mtaji wa kutosha aongezewe ili aanzishe shughuli nyingine aachane na kazi ya saloon ya kike.
Furaha na tabasam lake limekuwa sababu ya kuvutia wateja katika saloon yake licha ya changamoto anazopitia.
Licha ya kutoeleweka katika jamii na familia yake anasema hakuwahi kukata tamaa wala kufikiria kuiacha kazi yake, anasema kazi hii anaipenda sana na anaifanya kwa furaha kwani anaona ni sehemu ya vipaji alivyojaliwa na Mungu na iwapo hatavitumia vyema anahisi atakuwa na deni mbele ya Mungu.
Pia amekanusha maneno ya watu wanaosema anafanya kazi hiyo kwasababu hana ajira serikalini au hana mtaji wa kutosha, Huseni anasema pesa anayoipata kwasiku mara siku 30 yaani pesa ya mwezi mmoja inaweza kumshinda mfanyakazi anayesubiri mshahara mwisho wa mwezi, kwani kwa siku moja hawezi kuondoka akiwa na pesa china ya sh.50,000/:
Hussen akiwa anakausha nywele za mteja kwa kutumia taulo baada ya kuziosha
MAONI
Anaishauri jamii na kusema kuwa kazi yoyote ambayo ni halali kutenda, tenda bila kujali maneno ya watu ilimradi unaifurahia kazi yako na inakupa kipato cha kumudu maisha yako, kitu cha muhimu ni kupenda kazi yako na kuifanya kwa moyo. Anasema maneno ya watu yasikufanye ushindwe kutimiza malengo yako na kufikia ndoto zako.
Reviewed by Beatha
on
December 05, 2024
Rating:




No comments: