DJM

DEUS BUGATU THOMAS. DJM/2024/1758

 KWANINI MWANZA HUITWA JIJI LA MIAMBA

Historia nyingi sana zimewahi kusimulia uzuri wa jiji hili, historia zingine zikisema ni jiji linalosifika kwa usafi lakini bado jiji hili linaonyesha utofauti mwingine wa kuitwa jiji la miamba ni kwanini?

Maeneo mengi sana na mji wa Mwanza yanazungukwa na mawe pengine ndiyo inaweza ikawa sababu kubwa ya jiji hili kuitwa jiji la miamba, si hivyo tu hadi katika ziwa Victoria baadhi ya sehemu kuna mawe ambayo yamejipanga kwa namna ya kustaajabisha sana na hata nchi kavu.


           Picha ya jiwe kubwa lililopo Mwanza, kiashiria cha jiji hilo kuitwa jiji la miamba. Picha na Deus Thomas


Asilimia 75 ya wananchi wa Mwanza wanaishi milimani na inaelezwa kuwa kwa kawaida umbali wa kutoka eneo la tambarare hadi kufika juu yamilima hiyo huanza mita 50 hadi 300


      Picha ikionyesha baadhi ya nyumba za wakazi wa Mwanza wanaoishi katika milima, tarehe 14, Disemba, 2024. Picha na Deus Thomas

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakazi wa mtaa wa Mabatini kusini na Mabatini Kaskazini, wakazi hao wameeleza sababu kubwa inayowafanya kuishi milimani ambapo wamesema kuwa, wanakimbilia milimani kwasababu viwanja vinauzwa kwa bei nafuu kwani sehemu ya kujenga chumba kimoja unapata kwa Tsh. 200,000/=


Mkazi wa mtaa wa Mabatini ya kusini Aman Kajuna anasema watu wengi wanakimbilia kuishi maeneo ya milimani kwa sababu upatikanaji wa viwanja hausumbui tofauti na maeneo mengine

“mimi nina familia ya Watoto wanne tunaishi huku juu kwa muda mrefu, lakini chanz cha kuja kuishi huku ni atiz la upatikanaji wa viwanja, ukitaka eneo zuri huwezi kupata kwa wakati, kwani kuna kuwa na mizungunguko mingi, lakini huku unapata kwa muda mfupi tena kwa bei nafuu” anasema Kajuna.



Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA imewahi kusema watu wanaojenga milimani wanapaswa kuchukua tahadhari, kwa kuangalia usalama wa ene husika ili kuepuka madhara yanayweza kujitokeza.

Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa Mabatini kaskazini Juma Mahega anasema tahadhari wanazozichukua kuhakikisha wanajiepusha na madhara ya kuishi milimani ni Pamoja na wanalazimika kuhama pindi ambcho hali ya hewa inapokuwa mbaya, mvua kubwa kunyesha ambapo inapelekea ardhi kumomonyoka kupitia maji yanayotiririka.



DEUS BUGATU THOMAS. DJM/2024/1758 DEUS BUGATU THOMAS. DJM/2024/1758 Reviewed by Deus on December 16, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.