HISTORIA YA BISMARCK ROCK
Kaskazini mwa tanzania kunakopatikana mkoani mwanza ambapo mkoa huu umekuwa ukijihusisha na uvivu na kilimo pamoja na ufugaji kwa uwepo wa ardhi iliyo na rutuba iliyopambwa na uwepo wa ziwa kubwa zaidi afrika ziwa Viktoria
Mkoani mwanza kumekuwa na vivutio mbalimbali kama kisiwa Cha sanane pamoja na jiwe la bismarck rock lililopo pembezoni mwa kivuko maarufu zaidi katika mkoa huu wa mwanza kivuko Cha kamanga feri ambapo abiria kutoka mjini kwenda upande wa pili wa sengerema.
Jiwe hilo la kamanga likionekana sambamba na ndege wanaopamba eneo hilo.Jiwe hili la bismarck rock limekuwa na historia kubwa katika nchi yetu ya tanzania na kuwa kivutio Cha kuleta mapato katika sekta ya utalii nchini .
Bismarck rock ni makumbusho ya mwanamalunde mtawi wa wasukuma wakati anafukuzwa na wajerumani alikimbilia kwenye jiwe hili kuishi kwasababu wajerumani walikuwa wanataka watoe utawala wa utemi.
Na hapo juu ya jiwe Kuna nyayo za huyo mwanamalunde Hadi Leo hii jiwe Hilo lilikuwepo Toka zama hizo mungu pekee ndo aliumba jiwe hilo na humo ndani ya jiwe Kuna pango ambalo huyo mwanamalunde alikuwa akiishi na ndani ya pango hilo pako kavu kabisa hamna maji na Kuna kila ktu kama kitandan na vitu vingine.
Pia jiwe hilo linatumika kufanya matambiko mbalimbali kwa mfano wahindi wanakuja kufanya matambiko yao na wananchi tofautitofauti wanachukua maji ya pembezoni mwa jiwe hilo na kwenda kufanyia matambiko na Ibada mbalimbali.
Jiwe hilo likionyesha pembeni hapo wananchi wanapokwenda kuchukua maji kwaajili ya matambiko na Ibada zao .Jiwe hilo pia Lina miujiza yake kwenye Hilo pango la mwanamalunde Kuna sehemu pameandikwa na damu kabisa kwamba hapo ndio mwisho wako ingia ufanye mambo Yako na utoke haraka na usiendelee mbele na maneno hayo hayajulikani yaliandikwa na nani.
Picha inayoonyesha juu ya jwe hilo Kuna nyayo za huyo mwanamalunde.Bismarck rock jina hilo limetokana nam uunganiko wa maneno mawili ambayo ni Bismarck na rock ambalo bismarck lilikuwa ni jina la mtu ambae alikuwa ni kansela wa ujerumani kipindi Cha ukoloni ambapo rock ni mwamba ndipo walipounganisha maneno hayo mawili ndo hao wajerumani wakapachika na kupata neno moja ambalo ni bismarck rock .
Reviewed by Pappy girl
on
December 16, 2024
Rating:






No comments: