DJM

DJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALI


 KIJANA ANAEJISHUGHULISHA NA SANAA YA MITINDO YA NYWELE(MSUSI)

Kijana anaetambulika kwa jina la Johnson Kimaro mwenye umri wa miaka 28 ambae ameamua kujishughulisha na sanaa ya mitindo ya nywele yaani ususi anaepatikana maeneo ya Nganza ambapo kazi yake hiyo inamuingizia kipato katika kazi yake Pamoja na kuendesha familia yake licha ya kuwa anapitia changamoto mbalimbali kwenye kazi hiyo 

CHANGAMOTO ANAZOZIPITIA JOHNSON KIMARO

Licha ya ufanisi mkubwa anaoufanya Johnson katika kazi yake,pia kuna baadhi ya changamoto mbalimbali anazozipitia,ikiwemo ya kudharaulika katika jamii kwani watu wengi wanaamini kazi hiyo ni mahususi kwa wanawake tu kwani imezoeleka hivyo,pia mbali na hiyo jambo lingine ambalo linamletea shida ni kwa upande wa wasichana ambao hufanya nao kazi na kutaka kumpatia rushwa ya ngono(kimapenzi).

MAONI YA JOHNSON KWA VIJANA WENZAKE

Aidha kwa upande mwingine Johnson aliwahasa vijana wenzake kwa kuamini wanachokifanya na kupambania ndoto zao ili wafikishe malengo yao licha ya changamoto zote ambazo watakuwa wanazipitia,kwani kwa kila jambo changamoto ni lazima lakini tu yawapasa kuwa wavumilivu,vicheko na madharau wao kwao yawapasa kuchukulia kama funzo na kuzidi kuweka bidii zaidi kwenye kazi zao. 




DJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALI DJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALI Reviewed by Yaywuwuwwu on November 21, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.