Sio rahisi kueleweka Kwa haraka Kwani ni kitendo kisicho Cha kawaida Kwa wanaume, kazi ya ususi imekuwa ikifanywa na Wanawake lakini hivi Sasa watu wengi hawachagui kazi za kufanya wapo wanaume wanaojishughulisha na ususi akiwemo Zabloan Makoye mkazi na msusi maarufu mtaa wa Silvin.
Amefanya kazi nyingi bila mafanikio ndipo alipoamua kujihusisha na ususi kazi ambayo imebadilisha maisha yake
Picha ikionyesha Zabloan anavofanya kazi yake Kwa kujiamini
Umaarufu wake umetokana na kujishughulisha na kazi ambayo inaaminika kufanywa na Wanawake. Imekuwa changamoto Sana kwake kuonekana dhaifu Kwa wanaume wenzakekwani wanamdharau Kwa kujishughulisha na kazi hii.
Picha hizi zinaonyesha jinsi Zabloan anavofanya kazi yake pia anasema ni moja ya kazi anayoipenda Sana kutokana na kipato anachokipata.
Ikumbukwe kuwa hakuna kazi inayochagua jinsia ila juhudi zako ndio mafanikio yako ameyasema hayo Zabloan akitoa ushauri Kwa vijana hasa wa jinsia ya kiume kufanya kazi bila kuchagua wakiamini kuwa Ususi ni kazi ya kike.
Reviewed by Deus
on
November 21, 2024
Rating:




No comments: