DJM

BARAKA KAARE DJM/2024/3635

 DARAJA LA KIGONGO KWENDA BUSISI

Mwanza ni mkoa uliyo zungukwa na ziwa Victoria kwa asilimia kubwa.kutokana na jiji la mwanza kuzungukwa na maji Raisi wa awamu ya tano hayati dkt john pombe magufuli alizindua mradi wa daraja linalopita katikati ya maji kigongo kwenda busisi mnamo tarehe 25 mwezi wa pili mwaka 2020.

Muonekano wa daraja la kigongo Busisi njinsi lilivyo kwa sasa.

Daraja hilo linalopita juu ya maji ya ziwa victotia kuunganisha eneo la kigongo wilaya ya misungwi na busisi wilaya ya sengerema lina urefu wa kilomita tatu na itakuwa daraja la sita kwa urefu katika bara la afrika.

Picha ikionyesha ujenzi wa daraja la kigongo Busisi upande wa sengerema.

Daraja hilo limepewa jina la JPM kwa sababu ndiye muazilishi wa daraja hilo ambalo litaweka hurahisi wa kuvuka kwa miguu kutoka kigongo wilaya ya misungwi kwenda busisi wilaya ya sengerema ndio faida kuu ya ujenzi wa daraja la JPM.

Picha ikionyesha sehemu ya daraja upande wa kigongo misungwi.

Pia daraja hili la JPM litasaidia kwa kiasi kikubwa sana pamoja na kukomboa muda wa kuvuka eneo la kigongo kwenda busisi ambapo kwa sasa wananchi wanatumia vivuko kikiwemo kivuko cha MV misungwi pamoja na kivuko cha MV mwanza hadi kufika dakika tano kwa kutumia gari na dakika 15 kwa miguu.


Picha ikionyesha sehemu iliyosalia ili daraja liweze kufanya kazi ya kuvukisha.

Teknologia za kisasa na usanifu zinazotumika katika mradi wa ujenzi wa daraja hili ni fursa kwa wahandisi mafundi na waajiriwa wa ndani kujifunza kwa kupata ujuzi ambao utasaidia kutekeleza miradi mingine siku sijazo.


Picha linavyoonyesha urefu wa daraja njinsi lilivyo.

Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 95 na inategemewa disemba 30;2024daraja la JPM kigongo kwenda busisi litaanza kutumika rasimi kwa wakazi wa jiji la mwanza pamoja na wananchi walio karibu na eneo hilo.

BARAKA KAARE DJM/2024/3635 BARAKA KAARE DJM/2024/3635 Reviewed by Christopha on December 16, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.