DJM

LIGHTNESS COLMAN MLACHA DJM/2024/0187

  Utalii wa Jiwe la Bicmarck Rock lililopo Ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza

Picha ya Bicmarck Rock jiwe linalotoa tafakari kwa watu jinsi lilivyokaa juu ya mawe mengine.

Bicmarck Rock ni jiwe maarufu sana sio tu kwa wakazi wa jiji la Mwanza bali pia wageni kutoka nje ya Jiji la Mwanza na nje ya nchi wanaotembelea jiwe hilo kwa utalii

Picha ya jiwe la Bicmarck Rock likiwa juu ya mawe mengine bila kuanguka.

Jiwe hili liko juu ya mawe yaliyojipanga kwa ustadi mzuri sana na wa kupendeza uliopo ndani ya maji ya ziwa Victoria kana kwamba limepangwa na kundi la wabobezi kwa kutumia  vifaa vya kisasa vya ujenzi .Hivyo kulifanya kuwa maarufu katika Mkoa huu wa Mwanza.

Picha ya jiwe likionekana likiwa ufukweni mwa bustani ya Kamanga iliyopo ziwani Victoria jijini Mwanza

Mawe haya yanapatikana kwenye ufukwe wa ziwa eneo la Kamanga.Jiwe hili ni moja kati ya vivutio vya utalii vinavyopatikana ndani ya jiji la Mwanza lililojaliwa vivutio vingi ikiwemo hifadhi ya Taifa ya saanane ambayo ni hifadhi pekee inayopatikana ndani ya Jiji la Mwanza.

Picha hii ikionyesha jinsi jiwe la Bicmarck Rock linavyoonekana kwa mbele likionyesha kama alama ya kujumlisha.

Kutokana na upekee na umaarufu wa mwamba wa Bicmarck Rock sio tu wageni wanaofika Mwanza kutembelea eneo hilo , bali hata wenyeji hutumia mda wao wa mapumziko kuvinjari na kufaidi mazingira,hewa safi na upepo mwanana kutoka ziwa Victoria.

Picha ya eneo ambalo wageni na wenyeji Mkoa wa Mwanza wanapokuja kwa ajili ya utalii na kupumzika wakiwa wanatazama jiwe la Bicmarck Rock

Pia wapo wafanyabiashara hasa wa Boti ndogondogo zinazotumika kutembeza wageni katika maji hasa ya karibu ufukweni ,pia wajasiriamali wabidhaa mbalimbali na wapiga picha ya mnato ambazo zinawanufaisha katika maisha yao kutokana na uwepo wa mawe hayo.

Picha ikionyesha mtu akiwa ndani ya ziwa victoria akivua samaki mchana 

Baadhi ya wenyeji wa Mkoa wa Mwanza wanadai kabla ya jina la sasa la Bicmarck Rock jiwe hili lilijulikana kwa jina la Mwanamalundi ikiwakilisha jina la jemedari mcheza Ngoma maarufu na mganga wa jadi aliyejaa maajabu kutoka jamii ya Wasukuma aliyeonyesha uhodari katika mapambano dhidi ya ukoloni enzi hizo.


LIGHTNESS COLMAN MLACHA DJM/2024/0187 LIGHTNESS COLMAN MLACHA DJM/2024/0187 Reviewed by Light on December 16, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.