SANAMU YA SAMAKI KIVUTIO JIJINI MWANZA
Picha ya samaki aliye katikati ya jiji la mwanza, round about iliyopo barabara ya kenyata, ambaye ni sehemu ya utalii katika jiji la mwanza.
Moja kati ya kivutio na fahari ya jiji la mwanza kinachowavutia watu mbalimbali ni pamoja na uwepo wa round about ya samaki iliyopo barabara ya kinyata katikati ya mji wa jiji hilo. Uwepo wa samaki huyu ni kiashiria moja wapo kinachoonesha uwepo wa samaki wanaopatikana ziwa victoria na ni ishara ya shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa mwanza ambazo zinawanufaisha wakazi wa jiji la mwanza na Tanzania kwa ujumla.
Samaki huyu ni kumbukumbu ya mmiliki wa kiwanda cha samaki ndugu Vickfish(2009)
Pia uwepo wa picha ya samaki katika round about hii imekua ni sehemu ya vijana kujiajiri kwani eneo hili limekua likivutiakwa watu wengi kufika hapo na kupiga picha.
Kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika kupiga picha katika round about hiyo, vijana waliamua kuanzisha kikundi cha wapiga picha kinachoitwa Mwanza Nuru group, kazi hii inawanufaisha kiuchumi wanagroup hao.
Samaki huyu ni alama katika jiji hili na amekua maarufu na kuchochea hamu ya watu wa nje ya Tanzania na ndani ya Tanzania kutamani kufika mkoani mwanza na nisehemu pekee ya watu kufanya matukio mbalimbali kama vile kupiga picha za harusi na hata viongozi mbalimbali wanapofika Mwanza lazima wafike katika eneo hili kwani vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii imechangia kulifanya eneo hili lifahamike kwa watu wengi.
Lakini historia inasema kuwa samaki huyu ambaye ni sehemu ya utalii katika jiji la mwanza aliwekwa na mfanyabiasharaVickfish mnamo mwaka 2009, ambaye alikua mmiliki wa kiwanda cha kusindika samaki ambapo lengo kubwa la kuweka samaki huyo ilikua kutangaza biashara yake .
Reviewed by Beatha
on
December 16, 2024
Rating:






No comments: