Jionee maajabu ya Bismark rock jijini Mwanza
Picha ikionyesha muonekano wa fukwe ya kamanga feli mkoani Mwanza na ndani ya maji linaonekana jiwe la maajabu yaani Bismark rock
Bismark ni jiwe la maajabu na maarufu linalopatikana maeneo ya kamanga mkoani mwanza na nijiwe linalotambulisha mkoa wa Mwanza na zaidi ya hilo likapewa thamani kubwa hadi kwenye fedha , picha yake ipo kwenye noti ya shilling elfu moja ya kitanzania
Picha ikionyesha muonekano halisi wa Bismark rock ambalo ni jiwe maarufu mkoani Mwanza na lenye mvuto kwa Kila anaeliona
Historia inasema jina la Bismark ni jina la kiongozi wa kwanza wa kijerumani kufika na kutawala Tanganyika ambapo ilikuwa ni miaka ya 1880s na alipofika Tanganyika na kuzunguka maeneo tofautitofauti ya Tanganyika atimae akafika Mwanza na kufanikiwa kufika maeneo ya ufukwe wa ziwa Victoria mkoani hapo na kuliona jiwe hilo la kipekee na lenye mvuto na maajabu ya mungu makubwa ambapo kwa kipindi hicho inasemekana lilikuwa halipo ndani ya maji ila lilikuwa pembezoni mwa ziwa Victoria na mwanzoni lilikuwa linaitwa jiwe la kupiga pondo maana yake eneo la faragha na usibisho huo unathibitishwa na katibu mkuu wa machifu Tanzania ambae pia ni mwenyekiti wa machifu mkoa wa Mwanza Ndugu Alone Mkomongwa ambae anasema jiwe hilo kabla alijaitwa Bismark rock lilikuwa linaitwa jiwe la kupiga pondo ya eneo la faragha,ambapo watu walipatumia kama eneo la kufanya maombi kwa mungu wao walijibiwa Kila wapokuwa wanaomba .
Picha ikionyesha maji yalivyo zunguka jiwe la maajabu kama stori inavyoeleza katika maeneo ya kamanga feli mkoani mwanza
Lakini wengine wanasema kabla jiwe ilo halijaitwa Bismark lilikuwa linaitwa jiwe la Mwanamarundi ,likiwakilisha jina la jemedari mcheza ngoma na mganga wa jadi kutoka jamii ya wasukuma alieonesha uhodari mkubwa katika mapambano zidi ya wakoloni ,alijulikana kama Iguru Ugomoro maarufu kama Mbingu au Mwanamarundi na inasemekana lilitokana na miguu yake kuwa mhembamba na mrefu sana na wanasema alikuwa na urefu wa futi 12 jambo ambalo siyo la kawaida kwa mwanadamu kuwa mrefu kiasi hicho.
Picha ikionyesha jiwe kubwa linalopatikana katika fukwe za kamanga feli na mbele yake linaonekana Bismark rock jiwe la maajabu na lenye mvuto na muonekano wa kipekee
Na ni kwanini liliitwa jiwe la Mwanamarundi kwa sababu ilikuwa ni maeneo ambayo alipenda kutembelea kwaajili ya kucheza ngoma na kuonesha maajabu yake ambae inasemekana alikuwa na uwezo mkubwa wa kuamuru kitu chochote kifanyike na kilitendeka na miongoni mwa maajabu hayo ni mkuki sita iliyochomekwa kwenye jiwe ilo alama za unyayo wake na na sehemu ambapo alikuwa akilala na kukua japo historia inasema ni nondo sita na wala siyo mikuki kama watu wanavyosema ,na nondo hizo ziliwekwa na mjerumani wa kwanza kufika maeneo hayo Otto Van Bismark ambae alitaka kuliangusha jiwe hilo enzi za utawala wake .
Picha ikionyesha kingo za fukwe ya kamanga feli ambapo linapatikana jiwe la Bismark rock
Ni kwanini liliitwa Bismark rock ni kwa sababu ya uimara wake kwani kama linavyo onekana na ukiliangalia kwa ukaribu unaweza ukasema unaweza kuliangusha lakini siyo kweli na Otto Van Bismark aliliita Bismark kwa sababu alishindwa kuliangusha baada ya kutumia njia tofauti tofauti akijaribu kuliangusha zikagonga mwamba na historia inasema kiongozi huyo alikuwa anasema ananguvu za kufanya jambo lolote katika huu ulimwengu lakini alishindwa kuangusha jiwe dogo kama lile na ndio likawa mwanzo wa jiwe hilo kuitwa Bismark rock yaani mwamba imara kama alivyokuwa imara kiongozi huyo wa kijerumani hadi Leo ni jiwe maarufu mkoani mwanza na Tanzania nzima kwa ujumla na ni moja ya kivutio cha watali kinachopatikana mkoani hapo na hewe mtanzania usichelewe na wala usisubiri kusimuliwa nenda kajionee maajabu ya jiwe hilo.
Reviewed by Barakaaa
on
December 16, 2024
Rating:

.jpg)
.jpg)


.jpg)
No comments: