SANAMU YA SAMAKI IMEKUWA KIVUTIO KIKUBWA HAPA JIJINI MWANZA
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa thelathini na moja (31) ya Tanzania wenye Postikodi 33000 ambao unazaidi ya wilaya nane (8).
Mwanza ni mkoa unaopatikana kaskazini mwa Tanzania ambao unazaidi ya kilomita za mraba 19,592km² na wenye idadi ya wakazi Milion tatu laki sita na elfu tisini na tisa na mianane sabini na mbili ( 3,699,872) kwa mjibu wa sensa ya mwaka 2022.
Mwanza ni mkoa maarufu sana kwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na wakazi wake zikiwemo ufungaji, kilimo pia uvuvi. Wakazi wa mkoa huu ni kabila la Wasukuma kabila ambalo linawatu wengi zaidi Tanzania.
Mkoa wa Mwanza umepambwa kwa uwepo wa ziwa kubwa zaidi Afrika Victoria linalounganisha nchi tatu zinazounda umoja wa nchi za Afrika mashariki zikiwepo Kenya, Uganda pamoia na Tanzania.
Ziwa hili linafanya mkoa huu kukuza uchumi wa nchi kwa shughuli za usafirishaji, uvuvi wa samaki kama dagaa, fulu, sato, sangara na nyinginezo nyingi pia kilimo kama vile mahindi, mpunga, pamba pamoja na mihogo.
Mkoa wa Mwanza umebarikiwa na mwenyezi Mungu kwa kuwepo kwa vivutio vingi kama kisiwa cha sanane pia jiwe la Bismarck rock na vinginevyo vingi vivutio ambavyo vimekua vikikuza sekta ya utari nchini.
Lakini ndani ya mkoa huu kuna kivutio moja wapo cha round about ya samaki iliyopo barabara ya Kenyatta ambapo watu kutoka maeneo tofauti tofauti ya Tanzania wanapta nafasi ya kupiga picha ya kumbukumbu na kuweza kufurahia muonekano wake ulivyo.
Sanamu hili la samaki hutema maji yanayofanya eneo hilo kuwa moja ya sehemu ya kufurahia na kupunguza mawazo kwasababu ya aina ya utemaji wake wa maji.
Sanamu hii ya samaki imetengenezwa na kampuni ya Vicfish na ilikuwa atengenezwe samaki aina ya Sangara ambae anapatikana ziwa Victoria lakini akakosewa.Badala yake akatengenezwa kichwa cha Sangara lakini kiwiliwili chake ni cha samaki Sato.Basi ikabidi abaki kama alivyo.
Pia katika eneo hili kunawatu wanaojipatia kipato kwa kupiga picha watu mbalimbali za kumbukumbu.
Shughuli za upigaji picha za kumbukumbu ukuendelea katika eneo hili la round about ambalo nimezungukwa kwa uwepo wa bustani yenye maua mazuri sana.Hakika round about hii ya samaki ni moja ya maeneo machache yanayoutambulisha mkoa wa Mwanza.
Sanamu hili hutambulisha aina ya samaki wanaopatikana katika ziwa Victoria.
Kalibu kanda ya ziwa, kalibu Mwanza, kalibu round about ya samaki kwa kufanya utari wa ndani kuweza kukua.
Reviewed by Christopha
on
December 16, 2024
Rating:

.jpg)



No comments: