DJM

MARIAM HASSAN DJM/2024/0158.

                          MPISHI

Amosi Kitongeje, mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa nyamalango ambaye anafanya kazi ya mapishi ya kupika chapati. Mapishi hayo ya kupika chapati alijifunzia kwa mama yake, nyumbani kwao alipolelewa, Amosi alikuwa akimtazama mama yake akipika chapati kwa ajili ya chai ya familia. 

Mara baada ya umri kusogea Amosi alihamwua kuchukua hatua ya kuondoka nyumbani kwao ili aweze kujifunza maisha ya kujitegemea mwenyewe. Mwaka 2020 ndipo rasmi kijana Amosi alihamwua ni kazi ipi aifanye ili aweze kujiingizia kipato ili asije kufa njaa. Akiwa katika mawazo ya kuwaza ni kazi ipi aifanye ndipo anakumbuka jinsi mama yake alivyokuwa akiandaa chapati, yeye pia anaona ni vyema yeye pia kupika chapati. 

Amosi alianza kujihusisha na upikaji wa chapati katika eneo la nyamalango ambapo alianza na mtaji wa TSHs 100,000/= hapo alinunua mafuta, jiko, vijiko, sahani na unga wa ngano. Ambapio alikuwa akiuza chapati 1@ kwa shilingi 300/=. Kazi hiyo Amosi anasema kuwa alikuwa akipata faida ambayo alikuwa akiitumia kwa ajili ya kujikimu yeye mwenyewe, kujenga nyumba lakini pia kuisaidia familia yake na wadogo zake pia katika kuwatimizia baadhi ya mahitaji yao ya shule.

Kijana huyu amedumu kufanya kazi yake katika eneo la nyamalango na sasa ni mwaka wake wanne na wteja wake wakubwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania na wengine ni wakazi wa maeneo tofauti tofauti yanayokizunguka Chuo cha SAUT. Kwa sasa, Amosi anajivunia sana kwa sababu kutokana na ngano kupanda bei amekuwa akiuza chapati 1@ kwa shilingi 500/= pia, amefanikiwa kuitanua kazi yake kwa kuongeza baadhi ya vyakula katika mgahawa wake ambapo anauza maandazi, chai na sambusa.

Licha ya kazi ya Amosi kuwa na mwendelezo mzuri wa utoaji huduma za kuuza chapati pia amewaajiri vijana wawili ili waweze kusaidiana nae katika kazi yake. Amosi pia anadai ya kuwa pamoja na kazi yake kumwuwezesha yeye kupata kipato bado anakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kodi kubwa ya eneo analofanyia kazi, kupanda kwa gharama za mahitaji ya mapishi na muda mwingine chapati kubaki.

Matamanio yake yeye anaamini kuwa kujitegemea kumempa akili ya kuweza kuelewa namna ya utaftaji wa maisha na anadai kuwa siku moja anatamani kuwa mfanya biashara mashuhuri.



Amosi akiwa katika mazingira yake ya kazi katika mida ya jioni katika eneo la nyamalango akiwa anasukuma chapatti kwa ajili ya wateja wake.



Hivi ndivyo kazi inavyofanywa katika eneo la kazi la Amosi, akiwa anageuza na kuhifadhi chapatti ambazo mimekwisha kuchomwa tayari.



Chapati hizi zipo tayari kwaajili ya wateja 

MARIAM HASSAN DJM/2024/0158. MARIAM HASSAN DJM/2024/0158. Reviewed by Pappy girl on December 05, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.