Uzuri wa fukwe ya Kamanga (Bismarck Rock) jijini Mwanza
Fukwe ya Kamanga inapatikana katika Jiji la Mwanza ikiwa ni moja ya maeneo mazuri ya umma kwa ajili ya wageni na wazawa kupumzisha.
Fukwe hii yenye upepo mwanana wa Ziwa Victoria ama Ziwa Nyanza kwa asili yake, inapambwa na mawe ya kuvutia na ya kustaajabisha ambayo yalipewa jina la 'Bismarck Rock' ikiwa ni asili ya jina la aliyekuwa kiongozi wa Ujerumani, Otto von Bismarck.
Mawe haya ni kivutio maarufu katika fukwe ya Kamanga, yakijulikana kwa ukubwa na umbo la kipekee huku yakihusishwa na simulizi tamu za asili ya watu wa Mwanza ambao ni kabila la wasukuma ambapo inaelezwa mwana utamaduni wa kabila hilo, Mwanamalundi alikanyaga kwenye mawe hayo na kuacha nyayo zake hadi leo.
Fukwe hii ni maarufu kwa matukio ya kijamii kama vile sherehe, mikusanyiko ya familia na tafrija za kiasili ambapo wakazi na wageni huitembelea mara kwa mara na kuchochea uchumi wa jamii na Taifa.
| Muonekano wa mawe ya Bismarck Rock katika ufukwe wa Kamanga jijini Mwanza. |
| Muonekano wa boti za kukodi ambazo watu huzotumia kufika kwenye mawe ya Bismarck kujionea uzuri wake. |
| Muonekano wa mawe ya Bismarck katika ufukwe wa Kamanga jijini Mwanza. |
| Muonekano wa mawe ya Bismarck katika ufukwe wa Kamanga jijini Mwanza. George Marwa DJM/2024/1972 |
George Marwa DJM/2024/1972
Reviewed by BMG Media
on
December 16, 2024
Rating:

No comments: